Monday, March 25, 2013

ELIZABETH T. MOSHI AMBAYE NI AFISA UTUMISHI WA WILAYA YA RUNGWE AFANYIWA SHEREHE YA KICHENPART NA WAMAMA WA TUKUYU MJINI ANATARAJIA KUFUNGA NDOA MWANZONI MWA MWEZI WA NNE JIJINI ARUSHA

ELIZABETH MOSHI AKIWASHUKURU WAKINA MAMA WA TUKUYU KWA KUMUAGA KWA SHEREHE ILIYOFANA NA KUFUATA MAADIRI
ELIZABETH AKIWA NA MPAMBE WAKE WAKIINGIA UKUMBINI
MWENYEKITI WA KAMATI AKIMSHUKURU BIBI HARUSI MTALAJIWA KWA KUJITUNZA NA KUFIKIA UTU UZIMA WA KWENDA KUOLEWA


KATI YA ZAWADI NYINGI ALIZOPEWA ELIZABETH MOSHI

MWL ELIZABETH SEKILE AMBAYE NDIYE MC WA SHEREHE AKIMFURAHISHA JAMBO ELIZABETH HA HA HA HA HA HA MWANAMKE KUTUNZA NDOA ( MIE NILIISIKIA KWENYE MKANDA WA VIDEO MAANA HUMO NDANI SIRUHUSIWI KUINGIA)

ALIYESHIKA CAMERA KULIA NDIO MKE WA BAROZI WENU KINGO YEYE ALIKUWA NDIYE KATIBU WA SHEREHE YA ELIZABETI AMABAYE NI AFISA UTUMISHI ANAYETARAJIA KUFUNGA NDOA MWANZONI MWA MWEZI WA NNE JIJINI ARUSHA.

................................................................................................................................................................

JAMBAZI SUGU LAUWAWA KWA KUPIGWA RISASI KWENYE HARAKATI ZA KUTEKA MAGARI MLIMA NYOKA JIJINI MBEYA

Mwili wa Jambazi sugu  Emanuel Blasius Mdendemi ukiwa umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya  Diwani akiangalia mwili jambazi lililouwawa na kikosi cha polisi Mbeya
Baadhi ya polisi na waandishi wa habari wakiwa nje yajengo la kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa Mbeya
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika Mkutano alioufanya na waandishi wa Habari Ofisini kwake ambapo alisema tukio hilo lilitokea  jana majira ya Saa 10(kumi) Alfajiri usiku wa kuamkia Machi 27, Mwaka huu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani akionyesha baadhi ya siraha alizokutwanazo jamabazi huyo aliyeuwawa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani akionyesaha hirizi iliyofungwa katika bunduki aliyokuwa anatumia jambazi huyo kama kinga katika matukio yake 
Hii ndiyo hirizi iliyofungwa katika bunduki aliyokuwa anatumia jambazi huyo jamani waganga wakienyeji acheni hizo kuwadanganya watu matokeo yake ni kuongeza uhalifu nchini hakika nao tutawashughulikia kwani wamekuwa chanzo cha uhalifu nchini hayo yamesemwa na kamanda Diwani

Kamanda Diwani akiongea na waandishi wa habari


MTU mmoja ambaye anasadikiwa kuwa ni jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi na Askari wa Jeshi la Polisi akiwa kwenye harakati za kuteka magari katika Eneo la Mlima Nyoka Jijini Mbeya baada ya kutokea kwa majibizano ya kurushiana risasi.
  
Jambazi huyo ni miongoni mwa watu waliokuwa wakitafutwa na Jeshi la Polisi Mkoani hapa akituhumiwa kuhusika na mauaji ya Askari Polisi mwenye namba G 68 PC Jafari yaliyotokea  Februari 6, Mwaka huu  katika eneo la Matundasi Wilayani Chunya.
  
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika Mkutano alioufanya na waandishi wa Habari Ofisini kwake ambapo alisema tukio hilo lilitokea  jana majira ya Saa 10(kumi) Alfajiri usiku wa kuamkia Machi 27, Mwaka huu.
  
Kamanda Diwani alisema kabla ya tukio majambazi wapatao wanne  tayari walikuwa wameweka mawe barabarani kwa nia ya kuteka magari ili wafanye uporaji katika eneo hilo la Mlima Nyoka ambalo limekuwa na matukio kadhaa ya watu kuporwa mali zao.
  
Alisema Jeshi la polisi baada ya kupata habari za kutegwa mawe, askari walifika kwa wakati kwa kuwa polisi walikuwa jirani na eneo hilo na kuweka mtego kwa kuwa majambazi hawakuwa wameonekana kwa wakati ule.
  
Aliongeza kuwa baada ya muda majambazi walipoona taa za gari walijitokeza tayari kushambulia lakini kabla ya hapo polisi walitoa amri ya kujisalimisha kinyume chake wakaanza kupiga risasi ovyo ndipo mashambulizi ya polisi yakafanywa.
  
Diwani alisema katika mapambano hayo alijeruhiwa jambazi mmoja kwa risasi kiunoni na ubavuni kulia na wengine watatu walifanikiwa kutoroka ambapo Marehemu alipowahishwa hospitali kwa matibabu daktari alibaini kuwa amekwisha fariki.
  
Alisema  jambazi huyo alikutwa na silaha moja SMG yenye namba  AB huku namba  nyingine zikiwa zimefutwa na magazine yake ikiwa na risasi ishirini na mbili (22) pamoja na mapanga mawili 2.
  
Aliongeza kuwa baada ya  Marehemu kufanyiwa upekuzi maungoni mwake jambazi huyo alikutwa na kitambulisho cha mkazi chenye namba B.0010453 chenye jina la Emanuel Blasius Mdendemi aliyezaliwa mwaka 1984 eneo la Matamba wilayani Makete Mkoa wa Iringa makazi yake ni Uwemba Mkoani Njombe.
  
“Jambazi huyu amebainika kuwa ni miongoni mwa majambazi waliokuwa kwenye mtandao wa majambazi uliokamatwa hivi karibuni kuhusiana na matukio waliyofanya Mikoa mbalimbali ikiwemo Mbeya,Njombe na Iringa.aidha amebainika kushiriki katika tukio la mauaji ya askari polisi PC Jafari wa kituo cha Mkwajuni – Chunya tarehe 06.02.2013.” Alisema Kamanda Diwani. 
 
Aliongeza kuwa  ufuatiliaji wa majambazi waliotoroka unaendelea kufanywa ambapo pia  anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za wahalifu hao azitoe bila kuchelewa kwa jeshi la polisi ili zifanyiwe kazi.

Pia  amewatahadhalisha majambazi na wahalifu wa makosa yeyote kuachana na uhalifu kwa kuwa ni biashara isiyo na faida badala yake wafanye shughuli halali kupata maendeleo ambazo fursa zake ni nyingi.
Picha na Mbeya yetu 
 
 ............................................................................................................................

Greetings from JBG – Kibanda & Wife.



Hope all is well.
Salamu nyingi saaana toka JBG!
I could not resist! Yes I cried! But Absalom is the same person I knew last two months! Amesimama! Mungu ni Mwema!!!
Anaomba watanzania wamwombee na amesema anaendelea vizuri kwa sasa…
Cheers,
Hoyce Temu.
KINGO TANZANIA INAKUTAKIA KILA LA KHERI NA  URUDI SALAMA NA KUENDELEA NA  MAJUKUMU YAKO YA KILA SIKU YA KUIJENGA NCHI YETU YA TANZANIA BILA KUKATA TAMAA.

No comments: